EDINBURGH, Scotland
ALIYEWAHI kuwa kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers, amejiuzulu kuinoa Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland.
Taarifa za Rodgers kuondoka zilikuja saa chache baada ya Celtic kutandikwa mabao 3-1 na Hoops katika mchezo wa Ligi.
Ameiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi baada ya kukusanya pointi 17, ikizidiwa nane na Hearts iliyokaa kileleni.
Sasa, baada ya kutangaza uamuzi huo, mabosi wa klabu hiyo wamemrejesha kwa muda kocha wao wa zamani, Martin O’Neill.
Rodgers mwenye umri wa miaka 52, alirejea Celtic mwaka 2023 na ameipa taji la Ligi Kuu mara zote alizokaa kwenye benchi.
O’Neill (73), aliwahi kuinoa Celtic kwa miaka mitano (2000-05) na kutwaa mara tatu ubingwa wa Ligi Kuu.
Published:


