23.5 C
New York

Kaze afurahia Kaizer kutinga makundi CAF

Published:

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
KOCHA wa Kaizer Chiefs, Cedric Kaze, amefurahi na kuwapongeza wachezaji wake baada ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Dobsonville mjini Soweto, Kaizer walivuka raundi ya pili na kuingia makundi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya AS Simba ya DRC.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Lubumbashi ulimalizika kwa suluhu, hivyo ‘Amakhosi’ wameingia makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013.
Akizungumza baada ya dakika 90 za mchezo huo wa marudiano wikiendi iliyopita, Kaze raia wa Burundi aliyewahi kuinoa Yanga, alisema: “Tumefurahi kufuzu na kuingia hatua ya makundi.
“Unaweza kuona mashabiki walivyofurahi. Tulicheza mchezo huu kuanzia dakika ya kwanza tukiwa na morali ya kufanikisha hilo…”
Mara ya mwisho kwao kuingia makundi miaka 12 iliyopita, waliishia hatua ya 16 bora, ambapo walitolewa na ASEC Mimosas kwa kichapo cha jumla ya mabao 3-1.
Kaizer watashuka dimbani Ijumaa ya wiki hii kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini dhidi ya Durban City FC utakaochezwa katika Uwanja wa Moses Mabhida.

Related articles

Recent articles