23.5 C
New York

Vurugu zamaliza ‘derby’, polisi wajeruhiwa

Published:

TEL AVIV, Israel
VURUGUGU kubwa za mashabiki wa Hapoel Tel Aviv na Maccabi Tel Aviv wameshambuliana na kusababisha mchezo kati ya timu hizo zenye upinzani mkali kushindwa kuchezwa.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wapinzani hao wa soka kukutana tangu Hapoel iliporejea Ligi Kuu baada ya kucheza Daraja la Kwanza msimu uliopita.
Pia, tukio hilo limekuja zikiwa ni siku chache tu tangu mashabiki wa Maccabi Tel Aviv walipozuiwa kwenda Uingereza kuitazama timu yao ikicheza na Aston Villa katika mchezo wa Ligi ya Europa.
Sasa, hata kabla ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Israel kuanza, mashabiki wa timu hizo walianza kurushiana vitu, yakiwamo mawe na chupa.
Hali hiyo ilisababisha polisi waingilie kati kwa kuwarudisha wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia.
Hata hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya na hatimaye vurugu hizo kusababisha mashabiki na baadhi ya polisi kujeruhiwa.
Akizungumzia tukio hilo, Msemaji wa polisi alisema vurugu hizo zimebabisha maafa makubwa, ikiwamo uharibifu wa miundombinu ya uwanja.
“Ni kutokana na hali hiyo, sasa timu, viongozi, na wwaamuzi wamefahamishwa kuwa Uwanja wa Bloomfield hautotumika kwa mechi za soka,” amesema.

Related articles

Recent articles