20.9 C
New York

Kane hashikiki, afikisha mabao 400

Published:

MUNICH, Ujerumani
STRAIKA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya England, Harry Kane, amefikisha mabao 400 katika soka la ngazi ya klabu.
Kane amefika hapo baada ya kufunga moja katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wa jana wa Bundesliga.
Alifunga bao hilo la kichwa katika dakika ya 22, likiwa ni bao lake la 22 katika mechi 14 alizocheza msimu huu akiwa na Bayern na England.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 ameshafunga mabao 104 katika mechi 107 tangu alipotua Bayern mwaka 2023 akitokea Tottenham.
Akiwa Tottenha, Kane alipachika mabao 280. Mabao mengine ni yale aliyofunga akiwa kwa mkopo katika klabu za Millwall (9), Leyton Orient (5) na Leicester City (2).
Katika mchezo wa jana, Bayern walipata bao jingine kupitia kwa Michael Olise, wakati Dortmund walifungiwa na Julian Brandt zikiwa zimebaki dakika sita.

Related articles

Recent articles