23.5 C
New York

Mancini kocha mpya Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA mkongwe raia wa Italia, Roberto Mancini, amewaambia watu wake wa karibu kuwa huenda akakabidhiwa mikoba ya kuinoa Manchester United.
Kwa sasa, kocha raia wa Ureno, Ruben Amorim, ameendelea kupitia wakati mgumu kutokana na matokeo mabovu ya Man United.
Mancini mwenye umri wa miaka 60, amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipoachana na Saudi Arabia mwaka mmoja uliopita.
Akiwa kocha wa Manchester City mwaka 2011, Mancini aliipa kwa mara ya kwanza timu hiyo taji la Ligi Kuu baada ya ukame wa miaka 34.
Aliondoka Etihad mwaka 2013 akiwa ameiongoza timu hiyo katika michezo 191, ambapo alishinda 113 na kufungwa 40.
Tangu alipoondoka Man City, Mancini amezinoa Galatasaray, Inter Milan, Zenit, pia akifanya kazi na timu za taifa za Italia na Saudi Arabia.
Hata hivyo, Mancini si kocha pekee anayehusishwa kutua Old Trafford kuchukua mikoba ya Amorim.
Gareth Southgate aliyeondoka timu ya taifa ya England na kocha wa Crystal Palace, Oliver Glasner, nao wanatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Man United.

Related articles

Recent articles