23.5 C
New York

Benitez akaribia kuajiriwa Ugiriki

Published:

ATHENS, Ugiriki
ALIYEWEHI kuwa kocha wa Liverpool, Rafa Benitez, anakaribia kutangazwa kuwa mkuu mpya wa benchi la ufundi la klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki.
Benitez, raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 65, hana kazi tangu alipoondoka Celta Vigo mwaka jana.
Mtandao wa Sport24 umeeleza kuwa kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid amewasili mjini Athens, Ugiriki, kukutana na Rais wa Panathinaikos, Giannis Alafouzos.
Aidha, taarifa zaidi zinaeleza kuwa endapo mazungumzo yatakwenda vizuri, basi atasaini mkataba wa miaka miwili utakaompa Pauni milioni 11.
Wiki mbili zilizopita, Benitez alionekana akiwa karibu zaidi na Rais wa klabu ya Nottingham Forest, Evangelos Marinakis, ambaye ni mmiliki wa wapinzani wakubwa wa Panathinaikos, Olympiacos.
Marinakis na Benitez walinaswa na kamera za uwanja wakiwa jukwaani wakati Panathinaikos ikimenyana na Arsenal katika Uwanja wa Emirates.

Related articles

Recent articles