LONDON, Uingereza
MKUU wa benchi la ufundi la Arsenal, Mikel Arteta, amemtaka Viktor Gyokeres kuachana na presha za nje ya uwanja na badala yake kuelekeza akili yake katika majukumu ya timu.
Arteta amekuja na ushauri huo baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Sweden kucheza mechi sita bila kupachika bao.
Mashabiki wa Arsenal walikuwa na matarajio makubwa na Gyokeres baada ya timu yao kuinasa saini yake majira haya ya kiangazi akitokea Sporting Lisbon.
Matumaini ya mashabiki yalitokana na mabao 97 aliyofunga katika mechi 102 alizocheza Sporting.
Kwa upande wake, Arteta amemkingia kifua nyota huyo akisema: “Ana mchango mkubwa kikosini. Anawapa msaada mkubwa wachezaji wenzake ndani ya uwanja.”
Arsenal inaendelea kuikosa huduma ya nahodha wake, Martin Odegaard, ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na majeraha ya goti.
Published:


