LONDON,Uingereza
OPERESHENI kubwa ya polisi nchini Uingereza imefanikiwa kunasa genge linalojihusisha na uhalifu wa wizi simu.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mtandao huo unahusika katika wizi wa simu zaidi 40,000 zilizoibiwa Uingereza na kupelekwa China mwaka jana.
Katika operesheni hiyo, polisi wamefanikiwa kuwakatama washukiwa 18 na kukamata simu zaidi ya 2,000.
Miongoni mwa waliokamatwa ni wanaume wawili raia wa Afghanistan, ambao wameripotiwa kuwa na umri wa miaka 30 kila mmoja.
Wakati huo huo, mtuhumiwa mwingine ni mwanaume mwneye umri wa miaka 29, ambaye ameripotiwa kuwa na umri wa miaka 29.
Ikumbukwe, operesheni hiyo inatanguliwa na ile ya wiki iliyopita. Polisi walikamata watuhumiwa 15, mmoja akiwa ni mwanamke raia wa Bulgaria.
Published:


