30.7 C
New York

Saliba mitano tena Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza
BEKI wa kati wa Arsenal, William Saliba, amefichua kuwa amesaini mkataba mpya wa miaka mitano klabuni hapo.
Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema ameongeza mkataba akiamini ataimarika zaidi na kuwa beki bora duniani chini ya kocha Mikel Arteta.
Kabla ya huu mpya, Saliba mwenye umri wa miaka 24, alikuwa na mkataba uliokuwa ukifikia ukomo mwaka 2027.
Kwa upande mwingine, uamuzi wa kubaki Emiratse ni habari mbaya kwa Real Madrid iliyokuwa ikipambana kuinasa saini yake.
“(Arteta) ni mmoja ya makocha bora duniani kwa sasa,” amesema Saliba na kuongeza: “Amenisaidia sana, yeye na wenzake wa benchi la ufundi, hivyo nafurahi kubaki nao.”
Arsenal ilimsajili mlinzi huyo mwaka 2019 akitokea Ligue 1 alikokuwa akiitumikia Saint-Etienne.
“Tangu alipojiunga na sisi, William ameimarika mno, amebeba majukumu na kujenga uhusiano mkubwa na mashabiki,” amesema Arteta.

Related articles

Recent articles