LONDON, Uingereza
CRISTIANO Ronaldo ndiye mwanamichezo aliyeingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka jana, akivuna mara mbili zaidi ya mpinzani wake, Lionel Messi.
Kwa mwaka jana pekee, Ronaldo anayekipiga Al Nassr ya Saudi Arabia alivuna kitita cha Pauni milioni 192.40.
Aliyeshika nafasi ya pili ni staa wa mchezo wa gofu nchini Hispania, Jon Rahm, ambaye aliingiza Pauni milioni 161.32 mwaka jana.
Nafasi ya tatu imeangukia kwa mshambuliaji wa klabu ya Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina, Messi, aliyevuna Pauni milioni 61.42.
Staa wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), LeBron James, anafuata akiwa na mapato ya Pauni milioni 94.87.
Wakati huo huo, orodha ya ‘top 5’ inakamilishwa na mpachikaji mabao wa zamani wa Real Madrid raia wa Ufaransa, Karim Benzema.
Mwaka jana, nyota huyo anayekipiga Saudi Arabia akiwa na kikosi cha Al-Ittihad alivuna kiasi cha Pauni milioni 78.44.
Published:


