15.8 C
New York

Mourinho aikomoa Fenerbahce, achota bil. 25/-

Published:

INSTANBUL, Uturuki
KLABU ya Fenerbahce ya Uturuki italazimika kumlipa Jose Mourinho kiasi cha Pauni milioni 7.7 (zaidi ya Sh bil. 25 za Tanzania) baada ya kumtimua kocha huyo raia wa Ureno.
Wakati huo huo, Rais wa Fenerbahce, Ali Koc, amefunguka sababu ya uamuzi wao wa kumfuta kazi ‘Special One’.
Mourinho (61), alifukuzwa baada ya Fenerbahce kufungwa na Benfica, matokeo yaliyozima ndoto ya klabu hiyo kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na Manchester United alitimuliwa akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake.
Ni kwa maana hiyo basi, sasa Mourinho atakuwa amekusanya Pauni milioni 89 katika ajira zote alizowahi kufukuzwa.
Kwa upande wake, Koc amezungumzia sababu ya kumtimua akisema ni kiwango kibovu cha timu yao chini ya kocha huyo. “Msimu uliopita, tulikosa aina yetu ya soka la kushambulia. Tulipokaa mezani, tukakubaliana kuwa mambo yangebadilika msimu huu.
“Msimu ulipoanza, mechi tano tu zilituonesha yale yale ya msimu uliopita. Siyo kufungwa na Benfica, bali kiwango chetu kilinikera,” alisema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img