16.1 C
New York

Everton yanogewa kumbakiza Grealish

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
MABOSI wa Everton wanaangalia uwezekano wa kumsajili moja kwa moja winga wao wa mkopo kutoka Manchester City, Jack Grealish.
Grealish amekuwa moto wa kuotea mbali akiwa na jezi za Everton, ambapo tayari ana pasi za mabao (asisti) nne katika mechi mbili pekee alizoingia kikosi cha kwanza.
Kiwango chake hicho kilimpa tuzo ya Mchezaji Bora wa Agosti kwa upande wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Kwa mujibu wa makubaliano yao na Man City, Everton watalazimika kulipa Pauni milioni 50 ili kumsajili moja kwa moja nyota huyo mwenye umri wa miaka 30.
Wakati huo huo, Everton italazimika kukubaliana na mshahara wake wa Pauni milioni 12 kwa mwaka.
Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo wa Everton kumudu gharama hizo, hivyo huenda staa huyo akarejea Etihad hapo mwakani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img