14.7 C
New York

Israel yaitangazia ‘kiama’ Gaza

Published:

JERUSALEM, Israel
WAZIRI wa Ulinzi wa Israel amesema watalisambaratisha eneo la Gaza endapo wapiganaji wa Palestina, Hamas, hawatasitisha mapigano.
Mbali ya kutaka lisitishe mapigano, pia Waziri huyo, Israel Katz, ameagiza Kundi hilo kuwaachia mateka wa Israel.
“Punde tu, milango ya kuzimu itakuwa wazi kwa wauaji wa Hamas na wabakaji kule Gaza endapo hawatakubaliana na sharti la Israel la kusitisha vita na kuachia mateka,” alisema Katz.
Kauli yake inakuja, huku tayari Israel ikiwa imeshatangaza mpango wake wa kuivamia Gaza, licha ya kukosolewa vikali na jumuhiya za kimataifa.
Mapema wiki hii, Hamas walikubaliana na ombi la Qatari na Misri la kusitisha vita kwa siku 60, pia kuachia nusu ya mateka wa Israel.
Hata hivyo, Israel kupitia kwa Waziri Mkuu wake, Benjamin Netanyahu, inaamini kuwa mateka takribani 30 wameuawa na Hamas ndani ya miezi 22 ya vita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img