11.6 C
New York

Salah aweka rekodi akibeba tuzo ya tatu PFA

Published:

LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA).
Salah (33), ambaye pia ni mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, anakuwa mchezaji pekee kuibeba tuzo hiyo mara tatu.
Nyota huyo amewapiku Alexis Mac Allister, Bruno Fernandes, Alexander Isak, Cole Palmer na Declan Rice katika kinyang’anyiro hicho.
Wakati huo huo, kiungo wa Aston Villa, Morgan Rogers, ndiye aliyeibuka kidedea katika kipengele cha Kinda Bora wa Mwaka.
Kwa upande mwingine, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate, amepewa tuzo ya heshima kwa mchango wake akiwa na kikosi hicho.
Msimu huo, aliibuka na tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu hiyo, pia akiibeba ile ya Mchezaji Bora wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (FWA).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img