13.1 C
New York

Uingereza yaporomoka viwango vya unywaji pombe duniani

Published:

LONDON, Uingereza

KIWANGO cha unywaji wa pombe nchini Uingereza kimepanda kwa asilimia 10 kwa kipindi cha hivi karibuni. Ulevi ni tatizo kubwa nchini humo, ambapo ni chanzo cha vifo 10,500 kwa mwaka.

Sasa, habari njema kwa mamlaka za Uingereza ni utafiti mpya unoeleza kuwa matumizi ya pombe yamepungua na kufikia wastani wa lita 10 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Hiyo inaifanya Uingereza kushika nafasi ya 25 duniani, huku utafiti ukibaini kuwa wastani wa matumizi ya kilevi hicho ni chupa 112 kwa mtu mmoja kwa mwaka. Marekani ni ya 28 kwenye listi hiyo.

Hata hivyo, kiwango hicho ni kidogo kwa Uingereza, ukilinganisha na takwimu za mwaka 2000, ambapo ilikuwa nafasi ya tisa, wastani wa lita 11 kwa mtu mmoja.

Kwa upande mwingine, takwimu mpya za Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) zinaonesha kuwa tatizo la ulevi wa pombe limeongezeka kwa kasi katika mataifa ya Jamhuri ya Ireland (29%), Ufaransa (25%) na Ujerumani (16%).

Lakini, kwa mujibu wa WHO, mataifa 92 kati ya 187 yaliyohusishwa katika utafiti yalionekana kupunguza matumizi ya pombe kwa mwaka 2022. Syria, ukilinganisha na mataifa mengine, imeporomoka kwa kiasi kikubwa zaidi, ikipunguza matumizi ya pombe kwa asilimia 93.

Wakati huo huo, mataifa saba (Afghanistan, Iran, Libya, Mauritania, Somalia na Sudan) yameendelea kuwa na kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya pombe.

Aidha, mtafiti Dk. Melissa Oldham amesema licha ya ongezeko hilo, unywaji wa pombe kwa vijana umeshuka kwa kiwango kikubwa katika mataifa yanayofanya vizuri kiuchumi.

Mathalan, kwa Uingereza, vijana walio wengi, umri wa kuanzia miaka 16 hadi 24, wameonekana kuachana na matumizi ya vinywaji visivyo na kilevi.

“Ni kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo vijana kubadili mtazamo juu ya ulevi, pia elimu ambayo imekuwa ikitolewa juu ya madhara ya pombe,” anasisitiza Dk. Oldham. “Vijana sasa wana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya pombe yanavyoweza kusababisha magonjwa ya saratani na ubongo.”

Dk. Oldham anaongeza kuwa pia vijana wanaona namna matumizi ya pombe yalivyoathiri uchumi wa ndugu, jamaa na marafiki katika jamii zao.

Vilevile, Dk. Richard Piper naye anakuja na mtazamo wake, akisema kushuka kwa kiwango cha matumizi ya pombe miongoni mwa vijana wa Uingereza kumetokana na madhara ya kiafya.

“Watu wanaachana na pombe kwa sababu wanaona inavyoathiri uwezo wao wa kutunza kumbukumbu, kukosa usingizi, au matokeo mengine ya kiafya wanayokumbana nayo,” anasema Dk. Piper.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img