6.4 C
New York

Rais wa Yanga akatwa uteuzi Jimbo la Kigamboni, Jemedali, Shafii Dauda mambo mazuri

Published:

Na Mwandishi Wetu

Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Saidi ameshindwa kupenya katika  uteuzi wa awali wa wagombea ubunge  Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wadau wengine wa michezo wakiwamo, Shafii Dauda na Jemedali Said wakipita.

Injinia Hersi jina lake halikuwepo kati ya wagombea sita walioteuliwa kwa jimbo la Kigamboni ambao ni Ponela Matei, Habib Mchange, Allan Sanga, Henjelewe, Ally Mandai na Francis Elias.

Kwa upande wa Jemedali ametishwa na Chama hicho katika Jimbo la Mtama, mkoani Lindi akiwa pamoja na Nape Nnauye, Jabir Chilumba na Meta Nahonyo wakati Shafii Dauda akiteuliwa Jimbo la Temeke, jijini Dar es Salaam akiwa na Mariam Nassoro, Dorothy Kilave, Bernard Mwakyembe, Fadhil, Leah Mwampishi na Mussa Ntulia.

 Wanamichezo wengine walipita  katika uteuzi huo wa awali, ni Msemaji wa Azam Fc, Hasheem Ibwe, Jimbo la Mwanga, wakati Revocatus  Chiponda ‘Baba Levo’ akipenya Jimbo la Kigoma.

Majina ya wateule katika majimbo mbalimbali  wa CCM, yamewasilishwa  kwa waandishi wa habari leo Julai  29, 2025 jijini Dodoma na  Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa  chama hicho, Amos Makalla.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img