18.4 C
New York

Kocha Chelsea hofu tupu

Published:

LONDON, England
KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca, amesema timu yake si miongoni mwa zinazoweza kutwaa taji la Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu.
Maresca ameyasema hayo kuelekea mchezo wao wa kesho wa nusu fainali dhidi ya wakali wa soka la Brazil, Fluminense.
Endapo watavuka kizingiti hicho, basi watavaana na aidha Real Madrid au PSG katika mtanange wa fainali.
Kwa kutazama aina ya wapinzani waliobaki, Maresca anaamini bado vijana wake hawana nafasi kubwa ya kutwaa taji la michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Alipoulizwa kama Chelsea ina nafasi ya ubingwa, kocha huyo alijibu: “Hapana, sidhani kama Chelsea ina nafasi.
“Nafikiri kwa sasa hakuna timu yenye nafasi. Timu zote zimefika hapa kwa kuwa zinastahili na zina ubora wa kufika fainali na kuwa mabingwa.”
Fluminense ni moja ya timu tishio, ambapo itakumbukwa kuwa iliweza kuziondosha Inter Milan na Al-Hilal.
Katika mchezo huo, Chelsea itawakosa Levi Colwill na Liam Delap waliolimwa kadi mbili za njano kila mmoja katika mchezo uliopita dhidi ya Palmeiras.
Wakati huo huo, Romeo Lavia naye atakosekana kikosini kutokana na majeraha, ingawa Moises Caicedo atarejea ‘mzigoni’.

Related articles

Recent articles