13.9 C
New York

Uvutaji sigara holela marufuku Ufaransa

Published:

PARIS, Ufaransa
SHERIA mpya nchini Ufaransa inapiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya fukwe, shule na maegesho ya magari.

Kwa mujibu wa sheria, atakayekiuka, basi atalazimika kulipa faini ya euro 135 (Sh 416,718 za Tanzania) hadi euro 700 (Sh 2,160,760 za Tanzania).

Msingi wa sheria hiyo ni kuwalinda watoto dhidi ya moshi wa sigara, ikielezwa kuwa wamekuwa wahanga wakubwa wa vifo chini humo.

Aidha, Sheria hiyo iliyoanza kufanya kazi wikiendi iliyopita inakata uvutaji wa sigara katika maeneo yenye watoto, hasa shuleni.

Hata hivyo, Sheria hiyo haijapiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo ya baa na migahawa, tofauti na ilivyofanyika kwa majirani zao, Hispania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img