21 C
New York

Simba yatua Dar na kauli ya kishujaa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Kikosi cha Simba kimewasili Dar es Salaam kikitokea Zanzibar kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi RS Berkane ambapo mashabiki wamejitokeza Bandarini kuipokea timu yao, huku Msemaji wa klabu hiyo, Ahmed Ally akisema kwa hatua waliyofikia wanajihesabu kama mabingwa wa Afrika

Amesema wameumia kukosa ubingwa wa michuano hiyo lakini hawana deni na wachezaji wao wala benchi la ufundi kwa sababu wametimiza majukumu yao na wamevuka malengo, hivyo wanajihesabu kama mabingwa wa Afrika.

“Matokeo ya kufungwa mpira wa miguu huwa ni matokeo ya kuumiza, kinachouma zaidi kombe lilikuwa uwanjani, kombe jipya limeondoka tumelikosa sisi Simba, tuna maumivu makali mno, lakini katika mioyo yetu sisi Wanasimba tunajihesabu kama ni mabingwa wa Afrika,” amesema Ahmed.

Keshokutwa kikosi hicho kitashuka dimbani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida BS kwenye Uwanja wa KMC.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img