Na Mwandishi Wetu
Kutokana na ushindi wa Pamba Jiji wa mabao 2-0 dhidi ya KenGold, umeishusha rasmi daraja Kagera Sugar ambayo kwa nafasi na pointi ilizonazo hata ikishinda mechi zake mbili zilizobaki haiwezi kuchomoka.
Kagera Suga ipo nafasi ya 15 na pointi 22, hivyo kwa mechi mbili zilizobaki hata ikishinda zote haiwezi kufikia alama 29 walizonazo Fountain Gate waliopo nafasi ya 14.
Pamba jiji imefikisha pointi 30 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka nafasi ya 14 katika Msimamo wa Ligi Kuu Bara. Timu hii yenye msikani yake jijini Mwanza ina matumaini makubwa ya kusalia Ligi Kuu kwa sababu imebakiza michezo miwili na yote itakuwa nyumbani dhidi ya JKT Tanzania na KMC.