14.6 C
New York

Bonanza la JWTZ la basketball, handball lafana Morogoro

Published:

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kupitia timu teule za mpira wa kikapu na mpira wa mikono limejivunia mafanikio ya bonanza la michezo waliloandaa kutokana na kuwa katika kuimarisha afya na mshikamano kwa washiriki.

Bonanza hilo siku moja lilifanyika Mei 6, 2025 kwenye viwanja vya Klabu ya Magadu, mkoani Morogoro likihusisha washiriki zaidi ya 200, kutoka timu za JKT, Ngome, Jeshi Stars, Morogoro Warriors, pamoja na timu ya wastaafu (veterans), waamuzi na viongozi wa michezo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa bonanza hilo, Meja Mohamed Kasui ambaye ni Rais Mteule wa Kamati ya Ufundi ya Basketball Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), amesema bonanza hilo limeandaliwa kwa ubunifu mkubwa na ni kielelezo cha mwelekeo wa JWTZ kuimarisha afya kwa njia ya michezo, sambamba na malezi ya nidhamu, usawa wa kijinsia.

Amesema pia kupambana na changamoto za kimichezo za miaka hii zinazowakumbwa wanamichezo wote kwa ujuma kama vile matumizi ya mihadarati , ukosefu wa mshikamano miongoni kwa wadau wa michezo, uhaba wa miundombinu ya kisasa, masuala ya afya ya akili na rushwa kwenye michezo.

Mgeni rasmi wa bonanza hilo alikuwa ni Meja Jenerali Mbaraka Mkeremy, ambaye pia ni mlezi wa timu teule za michezo hiyo ambapo aliwapongeza Kurugenzi ya Michezo Makao Makuu ya Jeshi kwa maandalizi ya uratibu na wadau wengine akiwepo Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la kujenga Taifa Jenerali Rajabu Mabele na Mkurugenzi wa Mikopo ( DILS) Kanali Kachwamba kwa kuwezesha kufanikisha tukio hilo.

Viongozi wengine waliohudhuria bonanza hilo ni Mkuu wa Shirika la Mzinga Brigedia Jenerali Seif Hamisi, Kanali David Luoga Mkurugenzi wa Michezo JWTZ, Kanali Mstaafu Damian Majare , Katibu wa Klabu ya Wakongwe ya Temeke Justice Mwasakyeni, Mwakilishi wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF),Michael Kadebe na Ofisa Michezo Manispaa ya Morogoro.

Kaulimbiu ya Bonanza ilikuwa: ‘Afya, Nidhamu na Ushirikiano Kupitia Michezo’

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img