Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzani(TFF), limetangaza uchaguzi mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora ambapo gharama za kuchukua fomu ya nafasi ya Mwenyekiti ni Sh 200,000.
Nafasi nyingine zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao wote gharama ya kuchukua fomu ni Sh 100,000.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Juni 7,2025 mkoani humo na fomu zitaanza kutolewa Mei, Mosi hadi 5, 2025 katika ofisi ya TAREFA.