24.2 C
New York

Madrid wajitosa kumsajili Ter Stegen

Published:

MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid imeanza harakati za kuinasa huduma ya mlinda mlango wa Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen.
Ripoti zinaeleza kuwa kocha wa Madrid, Xabi Alonso, ndiye anayekazania usajili huo na amewaambia mabosi wake kuwa anamtaka Mjerumani huyo.
Ter Stegen (33), ameanza kuhusishwa na mlango wa kutokea tangu zilipoibuka taarifa za kipa huyo kukorofishana na mabosi wa Barcelona.
Inaelezwa, tayari kuna mawasiliano yameshafanyika kati ya Alonso na Ter Stegen na huenda dili hilo likakamilishwa wiki chache zijazo.
Alonso, kwa upande wake, anaamini Ter Stegen atampa ushindani wa kutosha kipa wa kikosi cha kwanza, Thibaut Courtois.

Related articles

Recent articles