9 C
New York

Januari Makamba, Mpina wakwama, Nape avuka uteuzi CCM

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla amejata majina ya wagombea sita wa  Jimbo Bumbuli mkoani Tanga  ambapo  aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kipindi kilichopita  Januari Makamba jina lake halijapita.

 Makalla ametaja orodha ya majina ya wateule wa jimbo hilo watakaokwenda kupigiwa kura za maoni leo Julai 29, 2025, jijini Dodoma, ambao ni Hidaya Kilima, Zahoro Rashid Hanuna, Eng. Ramadhan Singano, Rashid Salimu, Silas Joram na John Aloyce.

 Naye aliyekuwa Mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu, Luhaga Mpina ameshindwa kupenya  katika  watiania  saba wa ubunge  wa jimbo hilo  waliopitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuingia katika mchakato wa kura za maoni ambapo waliopita ni Lusingi Makanda, Silinde Mhachile, Joel Mboyi, Madili Sakumi, Godfrey Mbuga, Elias Mambembela na Gambamala Luchuga.

 Aidha aliyekuwa kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko, amepenya katika katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, Jimbo la Tarime Mjini mkoani Mara akiwa miongoni mwa wagombea sita walioteuliwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img