LONDON, England
ALIYEWAHI kuwa mchezaji wa Arsenal, Jay Emmanuel-Thomas, amejiunga na AFC Totton, zikiwa ni wiki chache tu tangu alipotoka jela.
Jay alihukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.
Mshambuliaji huyo aliyeanzia soka katika ‘academy’ ya Arsenal, amerudi uraiani akiwa ametumikia miezi 10 tu ya kifungo hicho.
Jay, ambaye sasa ana umri wa miaka 34, alikamatwa na bangi zenye thamani ya Pauni 600,000 (zaidi ya Sh bil. 2 za Tanzania) akiwa katika Uwanja wa ndege wa Stansted.
Kwa mujibu wa taarifa za wakat huo, mzigo huo uliotajwa kuwa na uzito wa kilogramu 60 ulifika hapo ukiwa unatokea Bangkok, Thailand.
Published:


