WASHINGTON DC, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema tayari ana matajiri wake wanaoweza kuununua mtandao wa kijamii wa TikTok, ambao umepigwa marufuku nchini humo kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni sababu za usalama.
Marekani imeshaiwekea sharti kampuni inayomiliki TikTok, ByteDance, kwamba italazimika kuuza mtandao huo kabla ya Septemba 17, mwaka huu.
Akihojiwa na Fox News, Rais Trump alisema ana matajiri ambao wameonesha nia ya kuununua mtandao huo wa China.
Hata hivyo, ili Marekani iweze kununua mtandao huo itahitaji kibali cha Serikali ya China, jambo ambalo Trump anaamini Rais Xi Jinping hatoweka kizuizi.


