22.6 C
New York

Dk.Samia atoa agizo kwa wanaochuja wagombea, asema Magwajima yaachwe nje

Published:

Na Mwandishi Wetu

Mwenyewekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan,  amewataka wanaochuja wagombea wa uchaguzi watende haki na wapime kwa umakini na kuangalia wale wanaofaa ili kuepuka kupitisha ambao wanakosa sifa na kuendana na yale ambayo chama hicho kinataka.

Dk, Samia ameyasema hayo waakt wa  kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa leo Mei 30,2025, jijini Dodoma.

“Niwaombe,  au sijui  niagize,  vikao vinavyokwenda kuchuja wagombea wakatende haki, anayefaa aambiwe anafaa, asiyefaa tuseme huyu ana kasoro moja, mbili, tatu, hatufai kwa huko  mbela tunakokwenda.

“Tukitoa mwanya ndugu zangu,tukipitisha wanaotafuta tu na mie niwemo ndiyo tunapata wale wanaokwenda huko, chama kinakuwa Gwajimanised. Kwahiyo kwa vyovyote vile tusigwajimanised chama chetu, Magwajima tuyaache nje, hamna kuoneana aibu wala haya, CCM oyee.

‘Unajua kule Zanzibar kuna mtu aliimba, mcheza ngoma si yake lazima ataharibu, akasema hawi sawa na wenzake, yeye anakuwa majidhubu, majidhubu ni mtu ambaye hazimo, hazimo hivi. Kwahiyo ukicheza ngoma si yako utaharibu na utajulikana tu kwani lazima utasema mi siye jamani,ndiyo hayo yanayotokea. Kwahiyo twendeni tukachuje kwa ustadi mkubwa,”Dk. Samia. 

Aidha Dk. Smia amesisitiza umoja kwa wanachama wa CCM ili kuingia katika uchaguzi mkuu kwa nguvu moja.

“Wosia wangu kwenu ndugu zangu tunakwenda kuingia katika kipindi kigumu kipindi cha uchaguzi, katika kipindi tunachohitaji kama Chama cha Mapinduzi ni umoja, mshikamano na upendo ni kipindi hiki,’ amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img