22.6 C
New York

CCM yaahidi kukamilisha Katiba mpya, kuzalisha ajira milioni 8

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Katika utekelezaji wa Ilani Mpya ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2025/30, Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM Prof. Kitila Mkumbo ameeleza kuwa katika kudumisha demokrasia na utawala bora nchini, CCM itaielekeza serikali pamoja na mambo mengine, kuhuisha na kukamilisha mchakato wa Katiba mpya.

Prof. Kitila amebainisha hayo leo Mei 30, 2025 kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma, wakati akiwasilisha muhtasari wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Mwaka 2025/30, pamoja na kutaja vipaombele vya ilani hiyo.

“CCM inaamini katika misingi imara ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria ni muhimu katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu kama msingi mama wa shughuli za maendeleo. CCM pia inatambua mchango wa falsafa ya uongozi wa 4R katika kudumisha maelewano, mshikamano na umoja miongoni mwa wadau wa maendeleo nchini.” Amesema Prof. Kitila.

Amesema  pia itaielekeza serikali katika kuimairisha misingi ya demokrasia na kuboresha mazingira wezeshi ya wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa sambamba na kuweka mfumo wa kisheria katika kutekeleza falsafa ya uongozi ya 4R.

Aidha amesema  Serikali itasimamiwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, kuimarisha serikali za mitaa kama nyenzo ya demokrasia na maendeleo ya wananchi pamoja na kuimarisha uhyru wa asasi za kiraia na vyombo vya habari kama taasisi muhimu katika kuimarisha uwajibikaji na sauti za wananchi wa Tanzania.

Katika hatua nyingine amesema Chama kitaendelea kuisimamia serikali kuhakikisha kuwa inakuza na kuwezesha shughuli za kiuchumi zinazoanzishwa na kuendeshwa na watanzania ili kuwala fursa ya kuendelea kushiriki katika shughuli za kiuchumi nchini.

” Lengo la CCM katika miaka mitano ijayo ni kuzalisha ajira zenye tija zisizopungua Milioni nane katika sekta rasmi na isiyo rasmi. CCM pia inalenga kuo a kuwa nusu ya ajira hizo zinazalishwa katika sekta rasmi, kimsingi kila eneo la kipaumbele cha ilani ya CCM ajira kwa vijana imetiliwa mkazo katika kuendelea kupanua fursa za ajira kwa vijana na kuwawezesha wananchi kiuchumi.” Amebainisha Prof. Kitila.

Ameeleza kuwa  katika kutekeleza suala hilo, chama hicho kitaisimamia serikali katika kuanzisha programy maalum ya ujenzi wa mitaa ya viwanda vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao kwa kila mkoa na kila wilaya pamoja na kuwezesha wabunifu wanaoanzisha kampuni changa ikiwa ni pamoja na kuwapatia mitaji ya kuanzia, ujuzi, fursa za masoko na kuendeleza bunifu zao.

“Kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kimkakati kwa kuhamasisha uanzishwaji na kuimarisha makampuni ya vijana na Vyama vya Ushirika (SACCOS) vyenye kujiendesha kibiashara katika Halmashauri zote nchini ili yaweze kupata mikopo, mitaji na nyenzo kwa lengo la kuwezesha wananchi wengi zaidi wakiwemo wanaohitimu elimu ya juu na vyuo vya ufundi kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine katika kuwajengea vijana uwezo wa kuajirika nje ya nchi, Serikali ya CCM itaanzisha vituo vya mafunzo stadi kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika kushindana kupata fursa za ajira nje ya nchi (skills development centres for overseas employment).” Ameongeza Prof Kitila.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img