16.3 C
New York

Balozi Nchimbi akabidhiwa ‘kifimbo’ cha Mwalimu

Published:

Na Mwandhishi Wetu, Gazetini

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel  Nchimbi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kijijini Mwitongo, Wilaya ya Butiama na kukabidhiwa fimbo maalum na familia hiyo ya mwasisi wa Tanzania. 

Balozi Nchimbi ambaye yuko ziara ya kikazi ya siku tano katika Mkoa wa Mara, mbali ya kukabidhiwa zawadi hiyo, yeye pamoja na msafara wake, pia alipata fursa ya kuweka shada la maua na kufanya misa fupi kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere. 

Kiongozi wa Kabila la Wazanaki, Chifu Joseph Wanzagi, amemwambia  Balozi Nchimbi kuwa hicho ni kifaa cha kazi atakachotumia katika dhamana alizoaminiwa kutumikia Watanzania. Amesisitiza kuwa huwa wanafanya hivyo kwa kiongozi mwenye sifa zinazofaa.

“Tunakukabidhi fimbo hii. Huwa tunakabidhi kwa kiongozi tunayemkubali. Kwa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi utaitumia kuchapa na kuwarekebisha wale wote ambao wanataka kutatiza shughuli za uchaguzi kinyume na utaratibu wa Kikatiba,” amesema Chifu Wanzagi. 

Balozi Nchimbi ambaye ameambatana na mwenza wake, Jane Nchimbi, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Mara na Wilaya ya Butiama, pia alipata fursa ya kufanya mazungumzo na familia ya Mwalimu Nyerere, nyumbani hapo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img