6 C
New York

Ukraine yaua wanajeshi wawili Libya

Published:

TRIPOLI, Libya

WANAJESHI wawili wa Libya wamepoteza maisha katika shambulizi la Ukraine dhidi ya meli ya kivita ya Urusi iliyokuwa kwenye Bandari ya Benghazi.

Libya, kama inavyofahamika, imegawanyika pande mbili, ambapo upande wa Tripoli una serikali yake inayovutana na ile ya Benghazi iliyoko Mashariki mwa nchi hiyo.

Kiongozi wa Benghazi, Oussama Hamad, ameeleza kuwa wanajeshi wake wawili walifariki baada ya kujeruhiwa vibaya na shambulizi hilo la Ukraine.

Kwa upande wake, jeshi la Libya limeweka wazi kuwa halitopuuzia kilichotokea, na badala yake litalipiza kisasi katika wakati na eneo sahihi.

Katika hatua nyingine, Ukraine kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Andrii Sybiha, imesema haiishawishi nchi yoyote, ikiwamo Libya, kuingia kwenye vita vyake na Urusi.

Related articles

Recent articles