PRETORIA, Afrika Kusini
RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameepuka kesi ambayo ilitarajiwa kumkabili ya wizi wa Dola 580,000 [zaidi ya Sh bil. 1.5 za Tanzania].
Ramaphosa alikabiliwa na tishio la Bunge kumfungulia mashitaka ya kuiba fedha hizo na kuzificha kwenye maeneo yake, yakiwamo mashamba.
Mwaka 2022, mwanasiasa huyo alikabiliwa na skendo ya kuficha fedha hizo hadi kwenye masofa ndani ya shamba lake katika Jimbo la Limpopo.
Hata hivyo, Mahakama ya Kikatiba imeikosoa ripoti hiyo ya Bunge ikisema ilikiuka baadhi ya taratibu za kutaka kumfungulia kesi.
Kwa upande wake, mchambuzi wa siasa, Khanyi Magubane, amesema uamuzi uliotolewa na Mahakama ni ushindi kwa Ramaphosa kwani umemsafisha dhidi ya tuhuma hizo.


