MERSEYSIDE, Uingereza
KLABU ya Liverpool imeripotiwa kuiwania kwa nguvu zote beki wa kati wa Borussia Dortmund, Joane Gadou.
Gadou [19], alijiunga na klabu hiyo ya Bundesliga majira ya kiangazi yaliyopita akitokea RB Salzburg.
Katika mechi 10 za Bundesliga za Dortmund msimu huu, kinda huyo ameanza mara tisa, pia akitumika mara tano kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ripoti zinaeleza kuwa Liverpool imeungana na Manchester United na Arsenal katika mBio za kuiwania saini yake, kama ilivyo kwa Real Madrid na PSG.
Hata hivyo, mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo ana Dortmund unatarajiwa kufikia ukomo wake mwaka 2031.


