14.3 C
New York

Kocha huyu EPL atatimuliwa tu

Published:

LONDON, Uingereza

MWANDISHI wa habari maarufu wa stori za uhakika zinazohusu soko la usajili barani Ulaya, Fabrizio Romano, ametabiri kuwa Crystal Palace wako mbioni kumtimua kocha wao, Pierre Sage.

Ni wiki chache tu zimepita tangu kocha huyo alipoajiriwa na Palace kuziba pengo la mwenzake aliyefukuzwa, Oliver Glasner.

Palace wanaelekea kwenye mapumziko ya kalenda ya FIFA wakiwa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England [EPL].

Kukaa kwao mkiani katika msimamo wenye timu 20 kumekuja baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-1 na Liverpool wikiendi iliyopita.

Ripoti zinaeleza kuwa baadhi ya vigogo wa Palace wameanza kufikiria juu ya kumfuta kazi na kuajiri kocha mwingine.

“Pierre Sage yuko mbioni kufukuzwa na Crystal Palace wakati huu timu hiyo ikiwa inaburuza mkia,” ameandika Romano katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter].

Related articles

Recent articles