11.8 C
New York

Mourinho atwaa tuzo kocha bora La Liga

Published:

MADRID, Hispania

JOSE Mourinho wa Real Madrid ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu ya Hispania [La Liga] wa mwezi uliopita [Oktoba, 2026].

Mreno huyo amewapiga bao Diego Simeone wa Real Madrid na kocha wa Real Sociedad, Pellegrino Matarazzo, kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu.

Moja ya mechi bora za ‘Special One’ kwa mwezi huo ni ile ya El Clasico, ambapo wakiwa ugenini Camp Nou walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Barcelona.

Kylian Mbappe ndiye aliyekuwa shujaa wa Madrid siku hiyo, ambapo alifunga mabao mawili [Dk. 41 na Dk. 87] kuihakikishia timu hiyo pointi tatu muhimu.

Kichapo hicho kilikuwa cha kwanza kwa Barcelona baada ya ushindi wa mechi tisa mfululizo za La Liga msimu huu wa 20255-26.

Related articles

Recent articles