19.3 C
New York

Kane mkataba mpya hadi 2029

Published:

MUNICH, Ujerumani

RIPOTI zinaeleza kuwa straika wa kimataifa wa England, Harry Kane, amekubali kuongeza mkataba utakaombakiza katika klabu ya Bayern Munich hadi mwaka 2029.

Awali, ilielezwa kuwa pande mbili hizo ziko mezani na sasa kituo cha televisheni cha Sky Sports kinaweka wazi kwamba yameshafikiwa makubaliano ya mkataba mpya.

Taarifa hizo ‘zinazika’ tetesi zinazomuhusisha nyota huyo na mpango wa kuondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu. Barcelona imekuwa ikihusishwa naye zaidi.

Mkataba mpya huo, kwa mujibu wa Sky Sports, utaambatana na ongezeko kubwa la mshahara kutoka kwa mabosi wake wa Allianz Arena.

Wakati huo huo, nahodha wa Tottenham, Pedro Porro, huenda akajiunga na Barcelona kupitia dirisha dogo la usajili wa Januari, 2027.

Related articles

Recent articles