19.3 C
New York

Haaland kama kawa, avunja rekodi Ulaya

Published:

MANCHESTER, Uingereza

STRAIKA wa Manchester City, Erling Haaland, alifunga mabao mawili, licha ya timu yake kufungwa mabao 4-2 na PSG katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa usiku wa jana Oktoba 15, 2026.

Katika mechi hiyo, PSG ilitawala kwa kiasi kikubwa kipindi cha kwanza, ikipata mabao matatu kupitia kwa Desire Doue [Dk. 13], Ousmane Dembele [Dk. 15] na Vitinha [Dk. 32].

Dakika ya 53, Haaland alifunga bao la kwanza kwa upande wa Man City lakini PSG iliongeza jingine kupitia kwa Maghnes Akliouche [Dk. 62], kabla ya straika huyo raia wa Norway kufunga tena [Dk. 75].

Licha ya kupoteza mchezo, Haaland amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 60 ya Ligi ya Mabingwa akiwa amecheza mechi chache [60].

Ni kwa maana hiyo, Haaland anaifunika rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Lionel Messi, ambaye alifikisha mabao 60 akiwa ameshuka dimbani mara 80.

Kwa upande mwingine, Haaland anakuwa mchezaji mdogo zaidi [miaka 26 na siku 85] kufikisha mabao 60 kwenye historia ya michuano hiyo.

Vilevile, Haaland anakuwa mfungaji bora wa muda wote wa Man City [mabao 38] kwenye mashindano hayo ya Shirikisho la Soka la Ulaya [UEFA].

Kwamba sasa nyota huyo amempiku mkongwe Sergio Aguero aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo akiwa na mabao 36.

Related articles

Recent articles