MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, atabadilisha wakala baada ya huyu wa sasa kushindwa kukamilisha usajili wa kujiunga na Barcelona wiki chache zilizopita.
Ripoti zinaeleza kuwa Alvarez anatarajiwa kuachana na wakala Javier Pastore ambaye ni mchezaji wa zamani wa PSG.
Baada ya kutemana na Patore, straika huyo wa kimataifa wa Argentina anatarajiwa kumpa ajira wakala wa kiungo wa Rodri, Pablo Barquero.
Kwa mujibu wa taarifa, Alvarez na familia yake wamekubaliana kuwa Barquero ndiye wakala wa sasa wa kufanya naye kazi kwa sasa.
Barquero ndiye aliyesimamia dili la Rodri kujiunga na Barcelona baada ya misimu mingi ya mafanikio akiwa na Manchester City.


