17 C
New York

Rais Serbia ajiuzulu kuelekea Uchaguzi

Published:

BELGRADE, Serbia

RAIS wa Serbia, Aleksandar Vucic, ametangaza kujiuzulu, ukiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu maandamano makubwa ya wanafunzi nchini humo.

Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi yalilenga kupaza sauti na kukosoa utendaji kazi wa Serikali, hasa vitendo vya rushwa kwenye sekta ya umma.

Awali, viongozi kadhaa wa Serikali walijiuzulu ili kuzima presha lakini hatua hiyo haikufanikisha kutuliza hasira za waandamanaji dhidi ya Chama tawala, Progressive Party.

Baada ya kuachia urais, Vucic anajipanga kuwania nafasi ya Waziri Mkuu katika uchaguzi ujao. Hawezi kuwania urais kwani tayari ameshatumikia awamu mbili.

Vucic alitarajiwa kumaliza muhula wake mwaka 2027, hivyo hatua ya kuachia ngazi kipindi hiki imewashangaza wengi, licha ya kwamba alishasema tangu Julai, 2026.

Kwa mujibu wa Katiba ya Serbia, Uchaguzi wa Rais unapaswa kufanyika ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu baada ya kujiuzulu kwake.

Related articles

Recent articles