20.4 C
New York

Visual| Abiria wa safari za ndani waliosafiri na ndege za ATCL

Published:

Ni takribani miaka nane sasa tangu kufufuliwa kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mwaka 2015 na aliyekuwa Rais wa Awmu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Ikumbukwe kuwa wakati Dk. Magufuli akichukua hatua za makusudi za kufufua shirika hilo lilikuwa limesaliwa na ndege moja tu.

Hata hivyo, leo mwaka 2022 ikiwa ni miaka 8 baadaye, shirika hilo lina jumla ya ndege 11 ambazo sehemu kubwa ni mpya.

Awali baada ya kurejea tena katika biashara kwa ATCL hali ya biashara haikuwa ya kuridhisha.
Tovuti yetu ya www.gazetini.co.tz imekusaidia kujua mwenendo wa wasafiri wa ndani ya Tanzania waliotumia ndege hizo katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2019.

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ATCL ambapo zinaonyesha ongezeko la wateja wa ndani wanaotumia ndege kusafiri kadri miaka inavyozidi kusonga.

Pamoja na mafanikio hayo takwimu hizo zinaonyesha kuwepo kwa hali ya kusuasua kwa wateja katika robo ya kwanza ya kila mwaka inayohusisha mwezi Januari hadi Machi.

Unafuu umeonekana kuwapo katika robo ya mwisho ya kila mwaka ambapo wateja wamekuwa wakiongezeka kama ilivyoonyeshwa katika usanifu wetu hapo juu.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa takwimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 idadi ya abiria wa ndani waliosafiri kwa kutumia ndege hizo ni 1,339,670.

Mgawanyo wa takwimu hizo kwa kila mwaka unaonyesha kuwa kwa mwaka 2015 kuanzia Januari hadi Desemba abiria waliosafiri na ndege hizo ni 52,145.

Mwaka 2016 walikuwa abiria 44,893, mwaka 2017 abiria 203,274, mwaka 2018 abiria 338,286 na mwaka 2019 walikuwa abiria 701,072.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img