MIAMI, Marekani
NAHODHA wa timu ya soka ya Taifa ya England, Harry Kane, amempiku mkongwe wa soka la Brazil, Pele, kwa idadi ya mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Kane amempiga bao Pele baada ya kupasia nyavu mara mbili katika ushindi wa mabao 2-1 walioupata England mbele ya DRC.
Kwa matokeo hayo ya mechi ya hatua ya 32 Bora msimu huu wa Kombe la Dunia, DRC imeng’oka, huku England ikitinga 16 Bora.
DRC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Brian Cipenga, kabla ya Kane kufunga mawili na kufikisha mabao 13 tangu aanze kucheza michuano hiyo.
Kwamba anamzidi moja Pele ambaye alistaafu akiwa amecheza mechi 14 za Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, Kane anaendelea kushikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England kwenye mashindano hayo.


