27.8 C
New York

Drogba aibuka, alia na VAR

Published:

MIAMI, Marekani

LEJENDARI wa timu ya soka ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, ameeleza kusikitishwa na uamuzi wa VAR kuwanyima penalti.

Drogba anazungumzia mchezo wao wa hatua ya 32 Bora dhidi ya Norway, akisema walistahili penalti katika tukio la Nicolas Pepe kuangushwa kwenye boksi.

Katika mchezo huo, Antonio Nusa aliitanguliza Norway, kabla ya Amad Diallo kuisawazishia Ivory Coast.

Dakika za jioni, Erling Haaland aliifungia Norway bao la pili lililoivusha timu hiyo hatua ya 32 Bora.

“Ni aibu kwa penalti kutokutolewa kwa Nicolas Pepe. VAR ina kazi gani sasa?,” aliandika Drogba katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter).

Ni baada ya matokeo hayo, Norway watakutana na mabingwa mara tano, Brazil, katika hatua ya 16 Bora.

Related articles

Recent articles