MEXICO CITY, Mexico
MASHABIKI wawili wa kandanda wamepoteza maisha nchini Mexico wakati wakishangilia ushindi wa timu yao ya Taifa.
Tukio hilo limetokea baada ya Mexico kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ecuador katika mechi ya hatua ya 32 Bora.
Kwa mujibu wa mamlaka za Mexico, waliopoteza maisha ni mwanaume mwenye umri wa miaka 44 na binti wa miaka 19.
Taarifa ya mamlaka za afya zimeongeza kuwa tukio hilo lilitokea katika Mitaa ya Hamburgo na Lancaster.
Mamlaka zimeeleza kuwa mashabiki hao walifariki kutokana na msongamano wa watu takribani 1,000 waliokuwa kwenye shangwe hilo.


