18.8 C
New York

Zidane agoma Benzema kurudi kikosini

Published:

PARIS, Ufaransa

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane, amefunga mlango kwa straika mkongwe, Karim Benzema, kurejea kikosini, licha ya kukiri kuvutiwa naye.

Zidane ameweka wazi kuwa kwa sasa anaelekeza nguvu kubwa kwa wachezaji wenye umri mdogo akiamini wataisaidia Ufaransa kufanya vizuri.

‘Zizou’ mwenye umri wa miaka 54, ametangaza kikosi kitakachocheza mechi mbili zijazo dhidi ya Uturuki na Ubelgiji.

“Nilikuwa naye kwa miaka mingi ya mafanikio pale Madrid. Navutiwa naye. Amewahi pia kuitumikia vizuri Ufaransa lakini kwa sasa nataka kuona chipukizi wakiwa na timu ya taifa,” amesema Zidane.

Benzema hajaitumikia Ufaransa tangu alipocheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Croatia mwaka 2022.

Related articles

Recent articles