10 C
New York

Barcelona yawatega Bastoni, Alvarez

Published:

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA imewaweka kwenye rada zake mastaa wakubwa wawili, beki Alessandro Bastoni na mshambuliaji Julian Alvarez.

Bastoni wa Inter Milan anatakiwa kwenda kuziba pengo la beki wa kati, Inigo Martinez, aliyeondoka majira ya kiangazi, mwaka jana.

Mkataba wake na vigogo hao wa Serie A utamalizima Juni, 2028. Barcelona watalazimika kuweka mezani Pauni milioni 51.

Kwa upande wa Alvarez wa Atletico Madrid, anatazamiwa kwenda kuvaa viatu vya Robert Lewandowski anayeweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, Atletico wameshaweka wazi kuwa hawako tayari kumpiga bei na endapo watalazimika, basi watahitaji si chini ya Pauni milioni 68.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img