16.3 C
New York

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa la kukataa bao halali la Simba wakati wa mchezo na Yanga ulichezwa Machi Mosi, 2026 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa leo baada ya kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kilichokaa Machi 4, 2026 kupitia mwenendo wa matukio mbalimbali ya ligi, mwamuzi huyo ambaye alikuwa msaidizi namba moja katika mchezo huo alishindwa kutafsiri vyema sheria za miguu.

Taarifa ya wataalamu wa kutafsiri sheria za soka baada  kufanyia tathmini ya video ya tukio imebaini kuwa hakukuwa na kola lolote kabla ya kufungwa kwa bao hilo.

Naye mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo huo, Hamdan Said kutoka Mtwara amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kusimamisha mchezo katika dakika ya 61 ya mchezo, akisimamisha shambulizi Yanga dhidi ya Simba kwa kuashiria kimakosa kuwa mchezaji Prince Dube alikuwa katika eneo la kuotea.

Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img