12.6 C
New York

Nkunku mguu mmoja Bayern Munich

Published:

MUNICH, Ujerumani
MATAJIRI wa Chelsea wameanza mazungumzo na Bayern Munich, ajenda kuu ikiwa ni mshambuliaji raia wa Ufaransa, Christopher Nkunku.
Blues wako tayari kumwachia Nkunku, ambaye Bayern wanaihitaji saini yake kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi.
Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya London inataka kumuuza Nkunku ili kupata fedha za kumsajili staa wa RB Leipzig, Xavi Simons.
Nkunku mwenye umri wa miaka 27, hana nafasi ya kuanza kikosini, hasa baada ya Chelsea kuwasajili Joao Pedro, Liam Delap, Jamie Gittens na Willian Estevao.
Juni, mwaka huu, kocha wao, Enzo Maresca, alikiri wazi kuwa nyota huyo atafungasha virago vyake na kuondoka Stamford Bridge.
Ni miaka miwili pekee imepita tangu Chelsea walipotumia Pauni milioni 52 kumsajili Nkunku na kumpa mkataba wa miaka sita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img