MERSEYSIDE, England
KIUNGO wa pembeni wa Liverpool, Federico Chiesa, amefichua kuwa matamanio yake ni kubaki klabuni hapo.
Wakati huo huo, Muitalia huyo amesema anajiandaa kukaa mezani na mabosi wa Liverpool ili kuzungumzia hatima yake.
Msimu wake wa kwanza Anfield, 2024-25, haukuwa mzuri kwani alicheza mechi sita pekee za Ligi Kuu.
Msimu huu ni kama Chiesa ameuanza vizuri baada ya kuingia kambani mara moja katika ushindi wa mechi yao ya kwanza ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bournemouth.
“Nafurahia kuwa hapa Liverpool. Nitazungumza na klabu lakini nataka kubaki na kupigania makombe,” alisema Chiesa akiwaambia waandishi wa habari.
Published:


