MERSEYSIDE, England
STAA wa Liverpool, Mohamed Salah, alishindwa kuzuia machozi yasimtoke aliposikia mashabiki wa klabu hiyo wakiliimba jina la aliyekuwa mchezaji wao, Diogo Jota, ambaye alifariki wiki chache zilizopita kwa ajali ya gari.
Mashabiki waliliimba jina la Mreno huyo baada ya kuishuhudia timu yao ikianza vizuri msimu huu wa Ligi Kuu ya England kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bournemouth.
Katika mtanange huo uliochezwa Anfield, Liverpool ilipata mabao yake kupitia kwa Hugo Ekitike, Cody Gakpo, Federico Chiesa na Salah.
Jota akiwa na kaka yake, Andre Silva, walipoteza maisha Julai 3 baada ya gari walilokuwamo kuwaka moto.
Ikumbukwe, tukio hilo lilikuja zikiwa ni siku 11 tu zimepita tangu staa huyo alipokuwa amefunga ndoa na mpenzi wake wa miaka mingi, Rute Cardoso.
Familia yake ilikuwa uwanjani wakati mashabiki wakiimba jina lake.
Published:


