11.2 C
New York

Kounde aongeza mkataba Barcelona

Published:

CATALUNYA, Hispania
KLABU ya Barcelona imetangaza kumpa mkataba mpya beki wake wa pembeni raia wa Ufaransa, Jules Kounde, na sasa atabaki Camp Nou hadi mwaka 2030.
Kounde mwenye umri wa miaka 26, ameongeza akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa.
Nyota huyo amekuwa mchezaji muhimu kwa Barca tangu aliposajiliwa mwaka 2022 akitokea Sevilla.
Anaungana na orodha ndefu ya wachezaji wenye mchango mkubwa kikosini waliopewa mikataba mipya katika siku za hivi karibuni.
Miongoni mwa mastaa hao ni Ronald Araujo, Pedri, Gavi, Raphinha na mshambuliaji aliyekabidhiwa jezi ya Lionel Messi, Lamine Yamal.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img