15 C
New York

Guardiola: Ederson bado namba moja City

Published:

MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesisitiza kuwa bado Ederson ataendelea kuwa changuo la kwanza langoni msimu huu.
Guardiola amekuja na kauli hiyo licha ya tetesi zinazoendelea kumuhusisha kipa huyo na klabu za Uturuki.
Kwa mujibu wa ripoti, Ederson anajiandaa kujiunga na Galatasaray, ingawa Man City imesema haina mpango wa kumuuza Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 31.
Wakati huu Ederson akiwa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake, Man City imeripotiwa kuanza kumfukuzia kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma.
Pia, kupitia dirisha kubwa la usajili wa majira haya ya kiangazi, Man City ilitumia Pauni milioni 27 kumsajili kipa kutoka Burnley, James Trafford.
Alipoulizwa ni kipa yupi ataanza katika mchezo wa leo Jumamosi dhidi ya Wolves, Guardiola alimtaja Ederson.
“Kwa sasa, Eddy (ndiye kipa namba moja),” alisema Guardiola na kusisitiza kuwa kipa huyo yuko fiti kucheza mechi yao hiyo ya kwanza msimu huu wa Ligi Kuu ya England.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img